fB insta twitter

Ujumbe aliouandika Professor Jay baada ya Polisi nane kuuawa na majambazi

on

Siku chache tu zimepita tangu kuripotiwa kwa mauaji ya Askari Polisi wanane ambao walikuwa wanatoka kubadilisha lindo kabla ya kushambuliwa na watu wanaosadikika kuwa majambazi Wilayani Kibiti, Pwani.

Tukio hilo limegusa hisia za watu wengi ambao kwa namna moja wamezielezea hisia hizo kupitia vyombo mbalimbali ikiwamo mitandao ya kijamii ambapo mmoja ya watu walioeleza hisia zao ni pamoja na Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ambaye leo April 15, 2017 aliutumia ukurasa wake wa Instagram.

Nasaha Pevu ‘Hatuwezi kuishi kwa amani bila ya kuwa na Jeshi la Polisi imara na ili tuwe na Jeshi la Polisi imara , tunapasawa kuwa na jamii inayotoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi haswa kwenye nyakati ngumu kama hizi , hivyo ni matumaini yangu kuwa Wananchi wote hususani wa maeneo hayo yalipotokea mauaji watakuwa tiyari kutoav ushirikiano ili kuwabaini wahusika wa tukio hili baya.’ Godbless Lema (MB), Waziri Kivuli wa Mambo ya ndani.” – Professor Jay.

FULLVIDEO: Kauli ya Jeshi la Polisi kuhusu mauaji ya askari polisi nane. Bonyeza play kutazma.

 

Soma na hizi

Tupia Comments