Ni mara chache kukutana na mwanamke aliyefikisha miaka zaidi ya 60 akiendelea kupata kubeba mimba hasa katika miaka ya sasa ambapo uzazi kwa wanawake wengi umekua wa shida tofauti na miaka ya nyuma.
Kumekuwepo na matukio mbalimbali yanayohusu uzazi ikiwemo mama kujifungua watoto mapacha kwa siku tofauti na hata hospitali tofauti.
Leo kuna Stori nyingine inatoka kule Ujerumani ambapo unaambiwa bibi wa miaka 65, Annegret Raunigk amefanikiwa kujifungua watoto wanne mapacha, watatu wakiwa wakiume na mmoja wa kike.
Daktari aliyemzalisha mama huyo kwa njia ya upasuaji alisema watoto hao walizaliwa wakiwa hawajatimiza miezi sita baada ya kugikisha wiki 26 lakini walizaliwa wakiwa na hali nzuri kiafya ya kuendelea kuishi.
Mama huyo tayari ana watoto 13 na wajukuu saba na ameingia kwenye rekodi baada ya kuwa mwanamke mzee aliyefanikiwa kubeba mimba ya watoto wamacha wanne katika umri wake.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.