CEO wa lebo ya Bad Boy Entertainment (BBE) P Diddy amekuwa miongoni wa mastaa wakubwa kwenye muziki ambao kwa kiasi kikubwa wamenufanikiwa sana kupitia biashara… kama wewe ni shabiki wa P Diddy basi taarifa hii ikufikie mtu wangu, msanii na mfanyabiashara huyo ametangaza kuwa lebo yake ya BBE inaungana na Epic Records ya Marekani kwa dhumuni ya kufanya nae biashara!
Kwa mujibu wa mtandao wa Billboard, mkataba kati ya Bad Boy Entertainment na Epic Records utakuwa kwa dhumuni ya kusambaza album mbili mpya na za mwisho za P Diddy (two upcoming Puff Daddy albums,) pamoja na kupromote, kutafuta soko na kufanya mauzo ya album hizo mbili.
>>> ” kwa karne hii ya 21, P Diddy ni miongoni wa watu waliochangia kwa kiasi kikubwa sana kwenye industry ya muziki na mchango wake umekuwa ukionekana mara kwa mara kupitia vitu vingi. P Diddy ni mbunifu mzuri sana ambaye kusema kweli nina furaha kubwa kushirikiana naye safari hii”. <<< L.A Ried CEO wa Epic Records.
Japo P Diddy hajaweka wazi majina ya album hizo ila kwenye interview aliofanya msanii huyo alisema mpango huo upo njiani na very soon atatangaza kupitia vyombo mbalimbali majina na uzinduzi wa album hizo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM,TWITTER,FB, YOUTUBE