Headlines za usajili barani Ulaya zimeanza kuchukua nafasi wakati huu ambao Ligi Kuu mbalimbali barani humo zinakaribia kumalizika, mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta ameanza kuhusishwa na Fenerbahce ya Uturuki.
Mbwana Samatta ambaye kwa sasa anaichezea KRC Genk ya Ubelgiji ameanza kuhusishwa na club hiyo kutokana na uwezo wake licha ya kuwa maamuzi hayo ya Fenerbahce yanatajwa kushangaza wengi, Fenerbahce kwa sasa wanatafuta mbadala wa mshambuliaji wao Robin van Persie ambaye anaonekana kuchoka.
Samatta ambaye ana umri wa miaka 24 anatajwa kutazamiwa na Fenerbahce kumrithi Robin van Persie aliyewahi kuvichezea vilabu vya Arsenal na ManUnited ya England, wachezaji wengine wanaotazamiwa na Thomas Bruns, Theo Bongoda na Ridgeciano Haps.
CHANZO CHA HABARI HII: mwananchi.co.tz
VIDEO: Game haikuoneshwa Yanga vs MC Alger, nimeyanasa matukio na goli la Yanga FT 1-0