Ajali

PICHA 5: Toyota Corolla iliyoungua na kuua Kagera

on

Ajali iliyotokea jana usiku maeneo ya Izigo barabara ya Muleba-Bukoba imeua watu wawili; dereva na abiria wake kati ya watu watatu waliyokuwemo ndani ya gari hiyo.

Ayo TV na millardayo.com imempata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Augustine Ollomi ambaye amesema kuwa gari yenye namba za usajili T 767 AWV Toyota Corolla iliacha njia na kupinduka hali iliyopelekea kuwaka moto na kusababisha vifo vya watu wawili kati ya watatu waliokuwemo.
Aidha, Kamanda Ollomi amewataja waliopoteza maisha kwenye ajli hiyo kuwa ni dereva Martine Kalunzi, 33 na abiria mmoja ambaye amefahamika kwa majina ya Gerevace Gerald, 33 mkazi wa Izigo.

VIDEO: Serikali imetoa ripoti ya vifo vitokanavyo na ajali za bodaboda

Soma na hizi

Tupia Comments