Michezo

Soka la Tanzania lapata msiba wa hodari mwingine Mwanza

on

Ni siku 57 zimepita toka soka la Tanzania lipokeaa taarifa za kifo cha mchezaji wa timu B ya Mbao FC Ismail Khalfan aliyefia uwanjani kwa moyo kusimama, leo soka la Tanzania linapokea taarifa za msiba wa moja kati ya magolikipa mahiri.

Asubuhi ya January 30 2017 taarifa za kifo cha golikipa wa Kagera Sugar David Buruhani kupoteza maisha ndio zimeenea katika mitandao ya kijamii, Buruhani ambaye amefia hospitalini Bugando Mwanza inaripotiwa kuwa amefariki kwa tatizo la ini ila kabla ya hapo mwenyewe alikuwa anajihisi kama anasumbuliwa na Malaria.

Taarifa za kifo cha David Buruhani ambaye licha ya kufariki akiwa mchezaji wa Kagera Sugar, amewahi kuzichezea timu za Mbeya City na Majimaji, zinakuja ikiwa ni siku 57 zimepita toka Tanzania impoteze mchezaji Ismail Khalfan aliyefia uwanjani wakati wa mchezo dhidi ya Mwadui FC December 4 2016.

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments