Watu 30 wamefariki kutokana na mvua kubwa zilizosababisha mafuriko nchini Malawi, ambapo taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani iliyotolewa imesema kuwa idadi ya walioathirika inatarajia kuongezeka.
Msemaji wa Wizara hiyo anayehusika na udhibiti wa maafa, Chipiliro Khamula, amesema watu 124 wamejeruhiwa huku takribani wengine zaidi ya 200,000 wamelazimika kuhama makazi yao katika jumla ya wilaya 14.
Rais wa Malawi Peter Mutharika ametangaza tukio hilo kuwa janga la Kitaifa baada ya dhoruba kali kusababisha kuta za mito kubomoka na mafuriko kufunika vijiji hivyo.
Katika maeneo hayo umeme umekatika na huduma ya maji imekosekana, Rais Mutharika ameelekeza misaada ya dharura kupelekwa katika maeneo hayo yaliyoathirika na kuratibiwa kwa haraka huku akilitaka Jeshi la Malawi kusaidia katika zoezi la uokoaji.
LIVE MAGAZETI: Bajeti ya Uchaguzi, Mbowe afunguka, Baba Matatani kumbaka mwanae