Habari za Mastaa

R Kelly akutwa na hatia

on

Mwimbaji wa R&B, Robert Sylvester Kelly maarufu R Kelly amekutwa na hatia katika mashtaka yote yanayomkabili ikiwemo unyanyasaji wa kingono kwa Wanawake na Watoto, rushwa, utekaji nyara na biashara ya ngono.

R Kelly anadaiwa pamoja na mambo mengine anadaiwa kutumia umaarufu wake na utajiri wake kuwarubuni Wanawake kwa ahadi za kusaidia kazi zao za muziki, baadhi ya Mashuhuda (Waathirika) wameiambia Mahakama kwamba walikuwa chini ya umri wakati wakinyanyaswa kijinsia na R Kelly.

Hukumu ya R Kelly inatarajiwa kutolewa May 04,2022 na huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 10 au kifungo cha maisha gerezani.

WAMEIBA NYUMBA YA MWANAJESHI WA JWTZ, KAMANDA KINGAI AWANASA “WAMEKIRI, WAPO WENGINE 80”

Soma na hizi

Tupia Comments