Ni Mbunge kutoka Nzega vijijini ambae pia ni Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi Kigwangalla na Mbunge Chalinze Ridhiwani Kikwete kwenye hii post ambapo ishu imeanzia kwenye alichopost Dr. Kigwangalla.
Aliweka picha ya vijana wa Kitanzania wakionekana kupambania kupata kazi TRA ambapo iliripotiwa kwamba nafasi za kazi zilizotangazwa na TRA ni 400 lakini waliojitokeza ni zaidi ya elfu 30.
Sasa baada ya kuiweka hiyi picha Dr. Kigwangalla aliandika “Je, hii inaashiria ukubwa wa tatizo la ajira nchini ama ni kwamba watu wetu wanachagua sana kazi za kwenda? #NjeyaBox”
Baada ya picha hiyo kupostiwa kwenye Twitter ya Dr. Kigwangalla baadhi ya Watanzania walitoa maoni yao ambapo miongoni mwao ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete aliemuandikia >>> “Unaweza dhani unauliza swali kumbe nawe unakua sehemu ya wachochezi! Mh. Waziri unaweza kuwa hujui kusoma lkn picha inatoa jibu sahihi”
EXCLUSIVE: AyoTV yamtembelea Mzee Kikwete Msoga, asema ‘nanenepa siku hizi, mlikua mnanifuja” MTAZAME KWENYE FULL VIDEO HAPA CHINI
VIDEO: Simu Mzee Kikwete aliyompigia Ridhiwani baada ya kuona picha aliyopiga na Edward Lowassa, PLAY HAPA CHINI KUMTAZAMA MWANZO MWISHO
HAUTAKI KUPITWA??? Kuna hii APP MPYA YA MILLARD AYO kwa wewe wa ANDROID unaweza kubonyeza hapa moja kwa moja kwenda kui-download mtu wangu, HABARI ZOTE KIGANJANI MWAKO >>> APP MPYA BONYEZA HAPA