Baada ya kumalizika kupangwa kwa droo ya makundi ya fainali za mataifa ya Afrika 2019 (AFCON 2019) zitakazofanyika nchini Misri June 21 hadi July 19, huku Tanzania ikiangukia Kundi C lenye timu za Senegal, Algeria na Kenya, AyoTV imefanikiwa kumpata nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta kutokea Ubelgiji.
Samatta ameeleza kuwa alikuwa anafuatilia upangaji wa droo hiyo lakini ameona kuwa ipo fair kwa timu zote licha ya kuwa wengi wameanza kuipa nafasi ya Senegal na Algeria kutokea Kundi C ndio watakuwa na uwezo wa kutinga japo kwenye mpira lolote linatokea.
“Kusema ukweli mimi nilikuwa nafuatilia nilipoona group jana nafikiri kwangu mimi ilikuwa ni fair, kwa maana huwezi kwenda kwenye mashindano yale halafu ukategemea ukapata timu ambazo ni rahisi kwa sababu ukiangalia timu nyingi ambazo zimefuzu ni ambazo zina ubabe fulani hivi katika taifa letu tayari nafikiri ni fair group kwetu”>>>> Samatta
Kutokea Algeria, Morocco na Hispania Ulimwengu, Msuva na Chilunda kuhusu Kundi C AFCON 2019