Habari za Mastaa

Rapper Kanye West amchapa busu zito mpenzi wake mpya hadharani

on

Ni Rapper kutokea nchini Marekani, Kanye West ambae time hii amerudi tena katika vichwa vya habari baada ya kumbusu hadharani mpenzi wake wa sasa aitwae Julia.

Wawili hao wameuthibitishia umma na kuamua kuweka wazi mahusiano yao mbele ya waandishi wa habari.

Hapo awali Kanye West alikuwa kwenye mahusiano na  mzazi mwenzake, Kim Kardashian ambae baadae mitandao iliripoti wawili hao kuvunjika kwa penzi lao.

Sasa kupitia video hii wengi wamehoji na kusema huenda Kanye anaamua kurusha vijembe ama kumuumiza roho Kim Kardashian.

Kwa upande wa Kim ameonekana kuwa na ukaribu usio wa kawaida na mchekeshaji Peter Davidson ambapo inatafsiriwa kuwa huenda wawili hao wakawa wapo katika mahusiano.

.

.

.

.

.

.

MAJIBU YA NANDY KWA MENINA, BILLNAS AMUITA RIHANA WA VINGUNGUTI

Soma na hizi

Tupia Comments