Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna wa Polisi Thobias Andegenye ameonyesha kutorizishwa na ubora wa ujenzi wa soko la Mpakani mwa Burundi na Tanzania Mkalazi Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma na kuagiza Halmashauri kusimamia ujenzi vizuri na kwa ubora.
‘’Tazameni makenchi yalivyokaa kule ndani yani huyo fundi ningemuona nisingempa kazi ningekuwa Mimi, lazima tuhakikishe tunapata mafundi wa kweli na kupata thamani inayolingana na pesa yetu hakuna pesa ya bure hapa hata kama ni ya Mfadhili, naogopa mpaka kuingia’’ RC Andengenye