Kenya imetajwa kwenye Top Ten ya nchi Tajiri Afrika 2015, hiyo ni good news.. Zimebaki wiki kama tatu hivi ili tushuhudie Rais wa Marekani, Barrack Obama anatembelea nchi hiyo, hiyo ni good news.. lakini ziko story upande wa pili wa shilingi pia.
Kama wewe ni mtazamaji wa Taarifa za Habari kwenye TV za Kenya itakuwa umeshuhudia pia majanga ya pombe za kienyeji, wapo wanaofariki, wengine wanajikuta hali mbaya mpaka wanalazwa Hospitali, lakini bado kuna wengine wanaendelea kutumia vilevile!!
Moja ya vitu vilivyonishtua ni hii kukutana na chupa ya Pombe ambayo wanasema hata haijasajiliwa na inauzwa kama kawaida. jina lake je? >> Inaitwa ‘Rest in Peace Premium Vodka‘ na kuna picha ya Jeneza kabisa kwa chini yake.
Serikali ya Kenya haijaliacha hili lipite, Vikosi vya Wanausalama wako kazini kuhakikisha wanafanikiwa kabisa kumaliza tatizo la Viwanda vya Mitaani vinavyozalisha pombe za Kienyeji.
Hapa iko na list ya Viwanda na aina ya Pombe ambazo Serikali ya Kenya imezipiga MARUFUKU !!
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.