Leo Hekaheka inatokea maeneo ya Mbagala kuu, Dar es salaam ambapo kuna kijana mtaani amekuwa akiwakera wananchi wa eneo hilo kwa tabia zake za kumpiga baba wa bibti aliyekuwa akiishi naye bila sababu yoyote.
Kijana huyo alianza mahusiano na binti wa baba huyo na kuamua kuishi pamoja lakini kila wakigombana na msichana huyo amekua akienda kupiga baba mzazi wa msichana huyo ambaye amemchukua kinguvu na hata mahari hajamtolea.
Jirani amesimulia na kusema wamekuwa wakikerwa na tabia ya kijana huyo aitwaye Ben kwa tabia za kumpiga baba mkwe wake kwa kutumia bisibisi kila wakati anapogombana na binti yake.
Baba mzazi wa binti ameelezea na kusema kijana huyo amekuwa akidai kwamba amuheshimu na kuamua kunywa pombe kisha kuja na kuanza kumpiga akiwa na binti yake ambaye alikua akiwasuluhisha na kuamua kwenda kwenda polisi na kupewa RB ambapo mpaka sasa wanamtafuta.
Wasikilize hapa wakihojiwa…
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.