Michezo

Ishu ya Mahakama kuzuia ujenzi wa Uwanja wa Real Madrid…

on

bernabeu6

Mahakama kuu ya Madrid imezuia ujenzi wa kutanua na kuboresha  uwanja wa klabu ya Real Madrid wa Santiago Bernabeu hali ambayo itachelewesha mradi wa kuongeza uwanja huo ambao tayari ulitengewa fedha na ulikuwa tayari kuanza muda wowote.

Mabingwa hawa wa Ulaya waliandika kwenye mtandao rasmi wa klabu hiyo juu ya hatua hii iliyochukuliwa na mahakama huku wakiwapa moyo mashabiki kutokuwa na wasiwasi na maendeleo ya klabu hii ambayo yataendelea kama ilivyopangwa.

Real Madrid ilizindua mpango huu tangu mwaka 2012 na mwaka jana mwezi januari Rais wa klabu hiyo, Florentino Perez alizindua michoro na ramani ya uwanja huo utakapokuwa umekamilika ambapo lengo lilikuwa kuongeza uwezo wake wa kuchukua watu toka elfu 84 mpaka watu elfu 90.

Katika mradi huo pia kulikuwa na mango wa kujenga paa la kisasa linaloendeshwa kwa kutumia mashine maalum, hoteli zilizoko ndani ya uwanja huo pamoja na eneo la maduka ya kisasa ambapo mashabiki wangeweza kununua bidhaa kadhaa zinazohusiana na klabu hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa mpango huu kuzuiwa baada ya kuzuiwa na kamisheni maalum ya umoja wa ulaya kufuatia shutuma za Serikali ya Hispania kutoa msaada kwa klabu ya Real Madrid katika mradi huo kinyume na sheria.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments