Mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya UEFA Champions League kati ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid ulichezwa usiku wa May 2 katika uwanja wa Santiago Bernabeu, ikumbukwe huu ni mchezo ambao ulikuwa unazikutanisha timu za mji moja wa Madrid nchini Hispania.
Real Madrid katika mchezo huo wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0 yalifungwa na staa wao wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo dakika ya 9, 73 na 86 ya mchezo, Ronaldo baada ya kufunga hat-trick katika mchezo huo anaweka rekodi zaidi ya moja.
Kufunga kwa Ronaldo kumemfanya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Champions League kufunga zaidi ya magoli 50 katika hatua ya mtoano, Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza Champions League kufunga hat-trick mbili mfululizo katika hatua ya mtoano kwa michezo ya kufuatana alifunga na Bayern na leo dhidi ya Atletico.
Ronaldo pia anakuwa mchezaji wa kwanza katika historia kufunga magoli 20 katika mchezo wa Madrid Derby yaani dhidi ya wapinzani wao wa jadi Atletico wanaotokea jiji la Madrid, Real Madrid sasa wanakazi ya kutafuta sare katika mchezo wa marudiano ili waingilea fainali lakini kesho ni Juventus dhidi ya AS Monaco.
GOAL & HIGHLIGHTS: Simba vs AzamFC April 29 2017, Full Time 1-0