Club ya Simba SC kupitia kwa afisa habari wake Haji Manara imetangaza masikitiko yake baada ya kupokea taarifa za watu kutumia jina la club hiyo na kudanganya mashabiki wa Simba kuwa inafanya usajili wa wanachama wa Simba sambamba na kutoa kadi za uanachama.
Haji Manara ameeleza kuwa wamezipata taarifa hizo kuwa zimekuwa zikitokea sehemu mbalimbali hapa Tanzania ndani ya Dar es Salaam na nje ya Dar es Salaam, kitu ambacho sio kweli na hawakubaliani na udanganyifu huo unaoendelea kufanywa na wahuni wachache.
“Simba tumepata matatizo baadhi ya watu wamekuwa wanapita mitaani na sio Dar es Salaam tu kote nchini wakigawa fomu za uanachama wa Simba na kadi, kuna mamilioni ya watu wanataka kadi za uanachama wa Simba, kwa hiyo kuna wapiga fursa wanafanya ujambazi mtaani”>>>Haji Manara
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake