Rwanda baada ya mwaka 2018 kuingia mkataba wa miaka mitatu na Arsenal kutangaza Utalii, kwa ajili ya kupitia upande wa mikono wa jezi za Arsenal na kuandikwa “Visit Rwanda”.
Mkataba wa Rwanda na Arsenal uliigharimu Rwanda dola milioni 44.3 (Tsh Bilioni 101.8) lakini ndani ya mwaka huo 2018 ilifaidika kwa ikupata mapato ya dola milioni 88.3 (Tsh Bilioni 202.9) kupitia Utalii moja kwa moja.
Mwaka 2019 Rwanda imeingia tena mkataba wa miaka 3 na club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa kwa ajili ye kuendelea kutangaza utalii wao, ambapo kuanzia msimu ujao Rwanda ndio watakuwa wauzaji wa kahawa ya Rwanda katika uwanja wa nyumbani wa PSG (Parc de Princes).