Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mwimbaji R.Kelly anadaiwa kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 400 za Kitanzania kama kodi ya jengo analotumia kama studio mjini Chicago na mwenye nyumba wake ambapo amedai kuzitaka pesa hizo.
Mmiliki wa jengo hilo la kampuni ya Midwest Commercial Funding walipeleka barua Sony Music ambayo ni kampuni ya inayosimamia kazi za R.Kelly kwa lengo la kufidia deni lao. Inaelezwa kuwa kampuni ya Sony ndio inayoishikilia akaunti ya fedha za R. Kelly hivyo wameilipa kampuni ya Midwest kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 3oo za Kitanzania na kubakiwa na deni la kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 120.
Kampuni ya Widwest imeiomba Mahakama iwape ruhusa ya kuzichukua fedha zilizobaki kutoka kwenye kampuni ya Sony ili wamalizane moja kwa moja na mwimbaji huyo.
VIDEO: GOOD NEWS KWA MASHABIKI WA DJ FETTY KAFUNGUKA KURUDI TENA KUTANGAZA