Zaidi ya siku kumi zilizopita stori za kufungiwa kwa video mpya ya Sauti Sol kuonyeshwa kwenye vituo vya TV nyumbani kwao Kenya zilitoka kutokana na kudaiwa kuvunja maadili kwa kile kinachoonekana ndani yake.
Baada ya hapo Sauti Sol wakakaririwa wakisema ‘hatukupanga kuwa na wimbo utakaozua gumzo au kumkwaza mtu kama hivi bali ni dhihirisho la penzi, haikua tu tutoe wimbo ambao watu wangesikiliza na kuridhika bali kitu ambacho kingeonyesha hilo kwenye video, ni kweli tumepata maoni mabaya kutoka kwa Wanaume lakini tunawajibu kuwa usimchukie mchezaji’
News ya sasa ni kwamba kituo cha TV cha Channel O chenye makazi yake Afrika kusini ambacho ni kati ya vituo vitatu vikubwa vya burudani Afrika kikionganisha kazi za Wasanii kutoka kila nchi zikiwemo Nigeria, Tanzania, Ghana, South Africa, Uganda, Kenya na nchi nyingine kimeanza kuicheza video hii.
millardayo.com imeshuhudia video hii ikipigwa mara mbili na Channel O ndani ya dakika 300 kati ya saa tisa usiku na saa mbili asubuhi na hii haimaanishi kwamba Channel O huwa hawakatai video wakiona imevuka maadili bali hii naona iko kwenye vigezo wanavyovitaka.
Stori zote ni kazi yangu uzipate mtu wangu, jiunge na mimi niwe nakutumia kwenye Twitter facebook na instagram kwa kubonyeza hapa >>> TWITTER FB INSTA