Top Stories

Mwanamke mwizi aiba gari ya polisi baada tu ya kukamatwa…ilikuaje?

on

Katika hali ya kuchekesha kama si ya kushangaza hivi karibuni, mwanamke mmoja  huko Texas nchini Marekani aitwaye Toscha Fay Sponsler mwenye umri wa miaka 33 aliyekuwa amekamatwa na polisi na kufungwa pingu kisha kuwekwa kwenye gari ya polisi hao alijifungua pingu alizokua amefungwa na kuondoka na gari hiyo kwa mwendo wa kasi.

Kabla ya tukio hilo mwanamke huyo alikua amekamatwa kwa kosa la kuiba vitu dukani yaani wakati anafanya shopping na baada ya polisi kumkamata kwa kosa hilo na kumwingiza kwenye gari yao hiyo wakiwa wamemfunga pingu na askari hao kuendelea na shughuli zao nyingine, walishangaa kuona baada ya dakika chache gari yao inaondolewa na mwanamke huyo.

Maaskari hao walijaribu kukimbiza gari hiyo kwa kutumia gari nyingine na baada ya mwendo wa dakika ishirini mwanamke huyo alishindwa kuendelea kuendesha gari hiyo na ndipo maaskari hao walipomkamata na kumtia mbaroni tena.

Uliiona hii? Walioiba gari Kenya wamelirudisha wakiwa uchi wa mnyama

Soma na hizi

Tupia Comments