AyoTV

VIDEO: Baada ya Sheria ya Makosa ya Mtandao, Jamii media wameingia Mahakamani

on

Septemba Mosi, 2015 Tanzania ilianza kutumia sheria ya Makosa ya Mtandao licha ya kuwepo kwa mvutano na malalamiko kutoka kwa wananchi wanaotumia mitandao hiyo kwamba hawakushirikishwa kuijadili na kuichambua.

Jamii Media wameamua kufungua shauri Mahakama kuu kutaka kifungu cha 32 na 38 chasheria ya Makosa ya Mtandao viangaliwe upya, akizungumza kwa niaba ya Jamii Media wakili Shukuru Mlwafu ameeleza

Baadhi ya vifungu vya sheria ya kimtandao vinakiuka masharti ambayo yamewekwa na katiba hasahasa vinaingilia haki ya faragha ambayo wateja wetu wanayo kikatiba, njia pekee ni kufungua shauri la kikatiba kupinga vifungu hivyo na kuiomba mahakama ibatilishe na itamke kuwa vifungu hivyo ni batili ’ ;- Shukuru Mlwafu

‘kuanzia uchaguzi october 2015 kumekuwa na barua kadha wa kadha zinazotaka kupata taarifa za siri za wanachama wa mtandao wa  jamii forum kitu ambacho tunahisi hata mitandao mingine ya kijamii wanafanyiwa na kumekuwa na mashinikizo kadha wakadha wakitaka tutoe IP Address za wateja’

Unaweza kutazama Video yake hapa chini….

Tazama hii Video kujua mambo muhimu kuyajua ili usipatikane kwenye mikono ya Polisi …

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments