Ikiwa imebakia siku moja kuelekea usiku wa show ya miaka 15 ya Saida Karoli, mastaa wa Bongofleva na Taarabu Shilole na Khadija Kopa leo July 5, 2017 kupitia Leo Ten ya Clouds FM wameelezea jinsi wasanii wa kike wa Bongo wanavyoshuka kimuziki na kushindwa kusimama tena.
Khadija Kopa amedai kuwa wasanii wa kike wanashindwa kujiheshimu na hulewa sifa mapema kitu kinachosababisha kupotea kwenye muziki.
>>>“Mimi nina miaka 30 kwenye kazi hii ya muziki. Wasanii wengi wa kike wanapotea kwenye tasnia kutokana na nidhamu ya kazi. Wanalewa sifa mapema na kushindwa kujua nini wanapaswa kufanya ili kuendelea kuwa juu katika kazi yao.” – Khadija Kopa.
Naye Shilole amedai kuwa kulewa sifa na dharau za wasanii wa kike baada ya kupata majina pia huchangia kupotea kimuziki kwa kuwa wakishapata umaarufu wanaanza kujisahau.
>>>“Mimi pia naungana na mama Khadija katika kile kinachowaangusha wasanii wengi wa kike katika muziki wetu. Nidhamu ya kazi. Mtu akishapata umaarufu anaanza kulewa sifa na kujisahau. Anasahau kazi yake ndio ilimletea hao Mabuzi wanaomhonga, mashabiki wanaomfuatilia kila kona na inaenda mwishowe anapotea kabisa.
“Namsifu mama yangu Khadija Kopa, yeye na Saida Karoli ni mifano ya kuigwa kwa sisi ambao hatuna muda mrefu kwenye sanaa. Hata kama ukianguka, usikate tamaa, pambana na inuka tena kuhakikisha unarudi tena juu.” – Shilole.
VIDEO: “Watu wanadanga sana tu, Kwenye utamu nimeonyesha uwezo wangu” – LuluDiva
Ndoto ya Idris Sultan kwenda Hollywood mbioni kutimia?