Michezo

Sir Alex Ferguson awatembelea PSG leo

on

Kocha wa zamani wa Man United Sir Alex Ferguson leo ametembelea Lowry Hotel iiliyopo katika jiji la Manchester ilipofikia timu ya PSG ambapo usiku wa leo inacheza na Man City katika marudiano ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ferguson katika hotel hiyo alikaa kwa zaidi ya saa moja na inaripotiwa kuwa alifanya mazungumzo na Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi na Kocha wa PSG Mauricio Pochettino.

Kwa kawaida hotel hiyo imekuwa ikitumiwa sana na Man United katika mechi zake za nyumbani kabla ya Ferguson kuondoka na hata baada.

Soma na hizi

Tupia Comments