AyoTV

KRC Genk ya Samatta imeibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya KV Oostende, hili ndio goli la Samatta (+Video)

on

Headlines za mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania ambaye pia ni nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta kuzidi kufanya vizuri zinazidi kuongezeka kila kukicha ndani ya Ligi Kuu Ubelgiji akiichezea klabu ya KRC Genk.

Samatta amerudi kwenye headlines baada ya kocha wa klabu ya KRC Genk kumpa nafasi ya kucheza mechi dhidi ya KV Oostende. KRC Genk imeibuka na ushindi wa goli 4-0, lakini kama kawaida Mbwana Samatta alifunga goli la tatu la Genk dakika ya 77 baada ya kuingia dakika ya 77 kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis.

Goli la Samatta lilifungwa baada ya Samatta kutumia vyema pasi ya mshambuliaji wa kimataifa wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Neeskens Kebano. Goli hilo linakuwa goli la tatu kwa Samatta toka ajiunge na klabu ya KRC Genk.

Video ya goli la Samatta

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments