Habari za Mastaa

Kuhusu picha za Snura anazoonekana yupo kwa Mganga wa Kienyeji,hii ni taarifa yake.

By

on

IMG-20140320-WA0021Siku chache zilizopita kupitia blogs na website mbalimbali zilisambaa picha zilizokuwa zikimuonyesha Snura akiwa kwa Mganga wa Kienyeji akiwa kama anapatiwa maagizo na mganga,ambapo kwa picha hizo zipo baadhi kamshika jogoo zingine anaonekana yupo baharini anatupa kitu.

Maoni ya watu wengi na namna ya uandishi wa habari hiyo juu ya zile picha yalionesha Snura akifanya hivyo ili mambo yake yamnyookee,millardayo.com imepata picha hizo ambazo zilikua zimerekebishwa na kutolewa sehemu zinazoonyesha camera ambazo zilikua zikirekodi.

Hemed Kavu ‘Hk’ ambaye ndiye Meneja wa Snura amelisemea hilo>>’Kiukweli tumeshangazwa sana na picha hizo zilizosambazwa ambazo zime ‘editiwa’ na kutoa sehemu zinazoonyesha camera ili kumchafua msanii wangu aonekane anashiriki mambo ya kishirikina’

‘Ukweli wa zile picha ni baadhi ya vipande vya kwenye filamu ambayo Snura anaigiza sasa hivi na ni filamu ya Dotnata inaitwa Mlokole’.

Hizi ni baadhi ya picha zilizopo kwenye filamu hiyo.

IMG-20140320-WA0022

IMG-20140320-WA0020

IMG-20140320-WA0017

IMG-20140320-WA0016

IMG-20140320-WA0015

 

Tupia Comments