Kikao cha Rais Jakaya Kikwete na watu wenye ulemavu wa ngozi albino kilisababisha kutokea kwa stori nyingine baada ya walemavu hao kuingia kwenye hali ya kutokuwa na maelewano kati yao wenyewe wakati wakiwa wanajiandikisha katika eneo la mapokezi la Ikulu.
Mzozo wa walemavu hao ulitokea eneo la mapokezi ya Ikulu Dar ambapo wapo waliokuwa wameorodheshwa kwa ajili ya kuonana na Rais, lakini likajitokeza kundi jingine ambalo halikuwa kwenye orodha hiyo, ilipofika muda wa kuingia ndani vurugu hizo zilianza ambapo waliwazuia viongozi wasiingie ndani bila wao huku wakidai kwamba kwa sasa hawana viongozi.
Tafrani hiyo iliendelea kwa muda na kusabisha shughuli zote za mapokezi kusimama kutokana na kelele zilizosababishwa na walemavu hao hali iliyosababisha Askari waliokuwa eneo hilo kuingilia kati na kuwaambia watoke nje ya geti ili wakajipange.
Mara baada ya kutolewa nje ya geti la Ikulu walianza kurushiana maneno wao kwa wao huku wakimzomea Mwenyekiti wao na kuzuia asihojiwe na waandishi wa habari waandishi wa habari muda mfupi baadaye wakaanza vurugu ambapo maafisa wa usalama walifanikiwa kumuokoa Mwenyekiti huyo.
Maafisa usalama wa Ikulu waliwaagiza waondoke maeneo hayo lakini baadaye Mwenyekiti huyo aliwasiliana na wenzake ambao walikuwa kwenye orodha ya kuingia Ikulu na kufanikiwa kuongea na Rais Kikwete.
CHANZO: Habari ITV, March 5, 2015. Unaweza kuisikiliza hapa, bonyeza PLAY..