Waziri wa zamani wa Nishati na Madini Willium Ngeleja amesema mgawo wa umeme ulioikumba nchi wakati wa uongozi wake ulimpa wakati mgumu na kufanya akose usingizi.
Alisema kukosa usingizi huko kulitokana na sababu ya matatizo lukuki yaliyokua yameigubika TANESCO kwani hapakua na uwekezaji wowote uliokua umefanywa na Serikali ili kuimarisha huduma za umeme kwa wananchi.
Ngelaja alisema miundombinu mingi ya umeme ilikua imechakaa kiasi cha kuzidiwa sana na isingeweza kukidhi mahitaji ya umeme ya wananchi wote.
Alisema iliwabidi kubuni na kuanza kutekeleza mipango na mikakati ya muda mfupi,muda wa kati na muda mrefu ili kukabiliana na mgawo wa umeme kwa wakati huo.
MWANANCHI
Mabomu manne ya kivita yamekamatwa yakiwa yamehifadhiwa chini ya ardhi katika mji mdogo wa Daraja Bobu Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja na bomu moja likihusishwa na kutumika katika mlipuko uliosababisha kifo cha mtu mmoja katika Manispaa ya Unguja.
Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdun Omar alisema mabomu hayo yameingizwa Zanzibar kupitia mtandao maalum ambao umekua ukifanya vitendo vya uhalifu kwa kutumia mabomu hayo.
Alisema mtu huyo amekua akijihusisha na vitendo vya kuagiza,kuingiza na kuhifadhi mabomu ya kivita ya kurushwa kwa mkono ambayo yamekua yakitumika katika matukio mbalimbali.
Alisema Polisi bado inaendelea na uchunguzi ili kujua mabomu hayo yametengenezwa kiwanda gani na yameingia Zanzibar kutoka sehemu gani ili kuwabaini wahalifu zaidi.
MWANANCHI
Ni kama sheria hazipo ama wasimamizi wa sheria husika wamelala kwani kemikali hatari aina ya Mekyuri inauzwa bila udhibiti wala tahadhari za kitaalam katika migodi ya wachimbaji wadogo Wilayani Serengeti,Mara.
Mekyuri ama Zebaki ni kemikali ambayo inapigwa marufuku na Serikali kuingizwa nchini lakini zuio hilo ni kama halipo kwani inaingizwa nchini na wamachinga na wanunuzi wa dhahabu katika migodi hiyo midogo.
Baadhi ya wachimbaji katika migodi hiyo wamethibitisha kuwepo kwa biashara hiyo na kwamba kemikali za Mekyuri hutuzwa kwenye chupa za dawa za binadamu na mifugo na inasemekana inatokea nchini Kenya kupitia mpaka wa Sirari.
Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa amekiri kuzagaa kwa kemikali hiyo na kwamba zinaingizwa kwa wingi toka Kenya huku kukiwa hakuna elimu yoyote inayotolewa kwa watumiaji wake ili kuwaepusha na madhara yake.
HABARILEO
Wafanyakazi zaidi ya200waliokua wakifanya kazi Shirika la Reli Tanzania TRC hawatalipwa mafao yao baada ya kujitoa kwenye kesi ya kudai fedha hizo.
Imeelezwa kuwa wafanyakazi hao walikau na haki ya kulipwa mafao yao ya kustaafu lakini walijitoa katika kesi hiyo kutokana na kukimbia gharama za kesi na kukata tamaa.
Katibu mkuu wa Chama cha wafanyakazi wa Shirika hilo Erasto Kihwele alisema wafanyakazi hao zaidi ya200 walipojitoa katika kesi hiyo walibaki1500 ambao ndio walioshinda kesi lakini pia amesema wana nafasi ya kufungua kesi nyingine ya madai kwani vielelezo vyote vipo.
MTANZANIA
Mtoto Hassan Suleiman (6) amegundulika kufungiwa ndani na baba yake kwa miaka sita bila kutoka nje baada ya kikudni cha Walemavu cha TUNAWEZA jijini Mwanza.
Baba wa mtoto huyo ambaye anajishughulisha na kazi za ujenzi amesema amelazimika kumfungia ndani mtoto huyo baada ya mama yake mzazi kumtelekeza hivyo amelazimika kumfungia ndani mtoto huyo pindi anapotoka kwenda kutafuta riziki.
Aidha baba huyo amesema aliomba ofisi ya serikali za mitaa kuomba aandikiwe barua kwenda katika vituo vya yatima ili wasaidie kumlea lakini hawakumpa ushirikiano.
Baada ya chama hicho kupata taarifa hizo walimtafuta mtoto huyo ambapo wamesema kuwa watamlea na kumpatia huduma zote.
MTANZANIA
Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shy-rose Banji amesema msimamo wake kupinga mbinu za kumng’oa Spika wa Bunge hilo Magreth Zziwa ambapo amesema wanatumia mitandao ya kijamii kumchafua kuwa alitoa maneno ya kashfa kwa marais wa Kenya, Rwanda, na Burundi.
Amesema baada ya kampeni hizo kushindwa wabunge walikuwa wakisusia vikao wakati wameshachukua posho.
Kuhusiana na kashfa kwamba alifanya fujo kwenye ndege na kutukana kwenye basi amesema ni uzushi unaoenezwa zenye lengo la kumchafua.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook