Habari za Mastaa

Maneno aliyotoa Mbunge Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kuhusu muziki wa Tanzania sasa hivi anavyowaona vijana

on

Tunao wabunge kama Profesa Jay ambaye alitokea kwenye muziki lakini sasa hivi ni mbunge wa jimbo la Mikumi Morogoro, wiki iliyopita alisema mwaka anaweza akatoa ngoma mpya, March 15 katika exclusive interview na Amlifaya ya Clouds FM mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu ameeleza namna ambavyo muziki wa hip hop kwa sasa na kuhusu yeye kutoa ngoma.

Mimi bado mwanamuziki hata juzi nilikuwa studio narekodi ngoma mpya ambayo itasikika hivi karibuni, zamani tulikuwa tunajivunia mistarii lakini sasa hivi ni mambo ya Branding tu, kutoa video kali basi,” >>> Sugu

Muziki unakua sasa hivi unazaa matawi, mimi naheshimu vipaji vyote na ninachoshukuru ni kwamba muziki kama muziki wetu bado sanaa ya mistari ipo… na bado kuna watu kama Fid Q bado anakomaa mpaka leo juzi nimeona track yake mpya, hajahama… sanaa kama sanaa wako watu bado wanailinda lakini acha vijana wengine wafanye hustle kwenye aina nyingine za muziki kila mtu atavyoona itavyofaa‘ – Sugu

Kwenye sentensi ya mwisho Mr. II amethibitisha kwamba baada ya ukimya wa miaka mitano kwenye muziki ameingia tena studio kurekodi ngoma yake mpya baada ya mashabiki kudai sana atoe kitu kipya, ameona wakati umefika kujibu kiu ya mashabiki wake…. ‘nimerekodi ngoma mpya kwa Master J, wimbo sio wa siasa ni tambo za hiphop

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FBYOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments