Habari za Mastaa

Tonto Dikeh kathibitisha kwamba sio filamu pekeake, anafanya na muziki pia.. Hii ni mpya yake.. -‘Sugar Rush’ (VIDEO)

on

Tonto-Dikeh1-600x254 (1)

Tunaona Bongo wasanii wakitoka kwenye industry ya Bongo Movie kuingia kwenye muziki.. wengine wanatoka kwenye muziki na kufanya movie.. sio kitu kigeni pia wasanii kufanya vyote viwili.

Tonto Dikeh mkali mwingine kutoka Nollywood, Return Of Tatoo Girls ni movie aliyofanya na star Van Vicker pamoja na Ini Edo, na movie nyingine ni Miss Queen.

Tofauti na muziki Tonto Dikeh tayari ana hits zilizotangualia kusikika kabla hii ya leo.. iko Itz Ova na Crazically Fit aliyomshirikisha Terry G .. Safari hii kaachia ngoma ya Sugar Rush  kwenye video ndani ameonekana msanii D’Banj.

Video imefanywa na director Moe Musa… jamaa ambae alifanya pia video ya Ommy Dimpoz, Ndagushima.

Tumia dakika zako tatu kuitazama hapa kwa kubonyeza play…

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenyeTwitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribeYouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments