Top Stories

TOP 10: Nchi zilizo nje ya Afrika zinazotajwa kuwa na idadi kubwa ya watu weusi

on

Watu wengi hufikiri kuwa nchi yenye idadi kubwa ya watu wenye ngozi nyeusi nje ya Afrika ni Marekani lakini sio kweli bali zipo nchi ambazo zina idadi kubwa sana ya watu weusi nje ya Bara la Afrika.

10. Trinidad na Tobago

Ni Visiwa ambavyo inasemekana kuwa na watu zaidi ya Milioni Moja na Laki Mbili (1,200,000), idadi inayosemekana kuongezeka tangu watu hao weusi walipohamia katika karne za 16 na 17 wakati bado iko chini ya ukoloni wa Wahispania.

9. Uingereza (UK)

Huu ni muungano wa nchi kadhaa zikiongozwa na England ambao husemwa kuwa na watu weusi takriban 1,900,000. Inaelezwa kuwa watu weusi nchini humu wana elimu zaidi ya wazungu ikitajwa 27% ya watu weusi wamepata elimu ya Chuo ukilinganisha na 13% ya watu weupe ambao ndio wana elimu ya Chuo.

8. Venezuela

Nchi hii ina watu weusi wapatao Milioni 2.6.

7. Jamaica

Watu wenye ngozi nyeusi zaidi ya Milioni 2.9 wanatajwa kuwepo katika nchi hii ambapo ni moja kati ya nchi ambazo zinatajwa kuwa idadi ya watu weusi ni kubwa zaidi katika takwimu za watu wote nchini humo.

6. Colombia

Kati ya watu Milioni 48 katika nchi hii, 10% ambayo ni zaidi ya Milioni 4.8 ni watu wa rangi nyeusi.

5. Ufaransa

Watu weusi kwenye nchi hii wanaripotiwa kuwa zaidi ya Milioni 5. Wengi wao wana asili ya Afrika na Carribean.

4. Jamhuri ya Dominica

Watu weusi Milioni 7.8 wanatajwa kuwa sehemu ya raia wa nchi hii.

3. Haiti

Inaelezwa kuwa 95% ya idadi yote ya watu katika nchi hii ni weusi wakitajwa kufikia Milioni 9. Inaripotiwa pia kuwa nchi ya kwanza katika Mataifa ya Ughaibuni kuachana na biashara ya Utumwa.

2. Marekani

Kuna zaidi ya watu weusi zaidi ya Milioni 45 katika nchi ya Marekani na inatabiriwa kuwa idadi hiyo itaongezeka hadi kufikia Milioni 80 ifikapo mwaka 2060.

1. Brazil

Hii ni nchi inayotajwa kuwa na idadi kubwa ya watu weusi nje ya Bara la Afrika. Brazil inatajwa kuwa watu weusi wapatao Milioni 80.

MAHAKAMA IMEMKUTA NA HATIA YUSUF MANJI….

Soma na hizi

Tupia Comments