Wakiwa katika maandalizi ya mchezo wa marudiano ya michuano ya CAF Champions League dhidi ya TP Mazembe utakaochezwa April 13 2019 mjini Lubumbashi, kocha mkuu wa Simba SC Patrick Aussems na nahodha wa timu hiyo John Raphael Bocco wamekabidhiwa tuzo zao leo hii.
Aussems alishinda tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu Tanzania bara kwa mwezi March wakati John Bocco akishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi March, hivyo Aussems na Bocco wote wamekabidhiwa tuzo zao leo kutoka kwa mdhamini wa tuzo hizo Biko Sports.
Tuzo hizo zitaambatana na zawadi ya pesa kwa kila mchezaji na kocha, ambapo kila mmoja atazawadiwa Tsh milioni 1 kama zawadi kutoka Biko Sports, Aussems alishinda tuzo hiyo baada ya kuiongoza Simba SC mwezi March kushinda michezo yote mitatu ya Ligi Kuu waliyocheza mwezi March.
Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars