Ni miaka 10 imepita sasa toka kitokee kifo cha Mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson, kazi za staa huyo zilimfanya apendwe na ajulikane duniani kote kiasi cha kutunukiwa jina la “King Of Pop”, najua tulisikia kuwa jumla la kifahari la Michael Jackson lililopo Calfornia Marekani “Neverland Ranch” lipo sokoni.
Leo mitandao ya USA imeripoti kuwa nyumba ya staa huyo wa Pop aliyefariki 2009 akiwa na umri wa miaka 50, imerudishwa sokoni kwa bei rahisi, Neverland Ranch kwa sasa nyumba hiyo la kifahari inauzwa kwa dola milioni 31 wakati mwaka 2015 miaka minne nyuma iliwekwa sokoni kwa bei ya dola milioni 100 lakini haikupata mteja.
Sababu kuu ya nyumba hiyo ya kifahari kuuzwa na familia ya Michael Jackson inatoka kuwa hawana pesa ya kulitunza jumba hilo, kutokana na kuhitaji pesa nyingi kwa matunzo, Neverland Ranch zamani ilijulikana kama Zaca Laderas Ranch na sasa utahitaji dola milioni 31 ambazo ni zaidi ya Tsh Bilioni 72 ili kulimiki nyumba hiyo.
Video: Viongozi na Mastaa waliosafiri hadi Bukoba kumzika Ruge Mutahaba