Watumiaji wa huduma za mawasiliano wanashauriwa kujihadhari dhidi ya utapeli kwenye
mitandao ya simu za mkononi kama ifuatavyo:
1. Usitekeleze maagizo yoyote yanayohusu fedha kwa ujumbe wa maandishi hata kama
yanatoka kwenye namba ya mtu unayemfahamu. Mpigie aliyekutumia ujumbe kwa namba nyingine uzungumze naye.
2. Usitekeleze maagizo yoyote kutokana na ujumbe wa simu za mkononi unaokutaka
kutuma fedha kutoka namba ambayo mtumiaji wake unamfahamu na ambao
unakueleza kwamba simu yake ina hitilafu hivyo hawezi kuongea, au yuko kwenye kikao.
3. Ukipigiwa simu na mtu yeyote kuhusu masuala ya fedha, hata kama unadhani
unamfahamu mtu huyo; mpigie tena kwa namba yake nyingine unayoijua (kama ipo) au
ya mtu aliye karibu nae ili kuhakikisha kwamba ni yeye.
4. Usitoe maelezo yoyote kuhusu usajili wa namba yako ya simu, neno la siri au
kumbukumbu ya simu ulizopiga na ya miamala mingine au taarifa za binafsi kwa mtu
yeyote anayekupigia simu kutaka taarifa hizo. Tembelea ofisi ya mtandao husika kupata
ufafanuzi.
5. Ukipoteza simu au laini yako ya simu toa taarifa kwa mtoa huduma wako na Polisi mara
moja.