Michezo

Taifa Stars imewashindwa Libya leo, game ilikuwa upande wao

on

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars unaweza kusema kama wamechezea bahati ya mtende kufuatia kupoteza mchezo wao wa pili wa kuwania kucheza fainali za AFCON 2021 nchini Cameroon, 2-1 dhidi ya Libya.

Taifa Stars walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 17 kupitia nahodha Mbwana Samatta kwa adhabu ya mkwaju wa penati, baada ya beki wa Libya kumchezea madhambi Saimon Msuva katika eneo la 18, licha ya goli hilo Stars waliendelea kutoa matumaini kwa watanzania kufutia kuwa na hali nzuri ya umiliki wa mpira.

Upepo ulibadilika kipindi cha pili baada ya wajukuu wa Muhanar Gadaffi timu ya taifa ya Libya na kubadilisha mchezo na kupata mabao mawili dakika ya 68 kupitia staa wao Sand Masoud kwa penati baada ya muamuzi kuona vibaya na kudhani beki wa Taifa Stars aliunawa na dakika ya 81 Anias Saltou.

Tunisia wao wameendeleza dozi kwa kuifunga Equatorial Guinea goli 1-0 ugenini na kuufanya msimamo wa Kundi J uongozwe na Tunisia mwenye point 6, Libya point 3(head to head) dhidi ya Tanzania inambeba na Tanzania nafasi ya 3 wakiwa na point 3 na Equatorial Guinea wakiwa wa mwisho kwa kwa kuwa na point 0.

Soma na hizi

Tupia Comments