Hii imeripotiwa na kituo cha Televisheni cha kimataifa cha CCTV Africa kuwa kwenye hifadhi ya Taifa ya Tarangire ambayo iko kusini magharibi mwa Arusha Tanzania. Wakazi wa maeneo jirani na mbuga hiyo wamebuni njia ya kufukuza wanyama ili wasiharibu mazao yao na kuwafukuza mbali na makazi yao.
Unaambiwa wamekuwa wakitumia Kondomu kuzuia wanyama kama tembo kuharibu mazao. Imeelezwa kuwa wanatumia unga wa pilipili na kondomu kufukuza wanyama waharibifu. Njia hii imeelezwa kufanya kazi vizuri na pia imekuwa ikisaidia wanyama kutopata madhara.
Unaweza kuangalia kipande cha video hapa chini
ULIKOSA DHAMIRA YA SERIKALI KUHUSU NDOA ZA UTOTONI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI