Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro amewahimiza askari kutimiza wajibu wao kwa kuhakikisha wanatenda haki na kufuata taratibu zilizopo huku akisisitiza kuwa Jeshi la Polisi lipo kwa mujibu wa sheria na kamwe halijihusishi na masuala ya kisiasa.
IGP Simon Sirro amenukuliwa akisema “kuna baadhi ya vyama vya siasa wana ajenda ya kufanya vurugu ili uchaguzi usifanyike” .
“Kuna kikundi cha watu kinasema kitatangaza matokeo, mimi imenishangaza kidogo, tunajua NEC na ZEC ndio wanawajibika kutangaza matokeo, unaposema unatangaza matokeo sasa sijui mamlaka hayo unayapata wapi,niwaombe tu wanasiasa wafuate sheria” IGP Sirro