Mamlaka ya mawasiliano Tanzania ‘TCRA’ kwa kushirikiana na watoa huduma za simu nchini wameanzisha huduma ambayo itamuwezesha mtumiaji wa simu kuhama kutoka mtandao mmoja wa simu kwenda mwingine bila kubadili namba, huduma hiyo inatarajiwa kuanza March mosi Mwaka huu.
Leo February 23 2017 kupitia clouds 360 ya clouds TV, Kaimu Naibu Mkurugenzi maendeleo ya TEHAMA kutoka TCRA, Mhandisi Nehemia Mwenisongole amefafanua baadhi ya mambo katika zoezi la kuhama mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu.
"TCRA na watoa huduma wamekuja na huduma inayomuwezesha mtumiaji wa simu kuhama mtandao bila kubadili namba ya simu"-@TCRA_Tz @Clouds360Tz
— millardayo (@millardayo) February 23, 2017
"Ukihama mtandao unahama na namba ileile ikiwamo zile za mwanzoni zinazotambulisha mtandao uliopo"-@TCRA_Tz @Clouds360Tz
— millardayo (@millardayo) February 23, 2017
"Unapotaka kuhama mtandao bila kubadili namba ya simu unatakiwa uende kwa mtoa huduma wa mtandao unaotaka kuhamia"- @TCRA_Tz @Clouds360Tz
— millardayo (@millardayo) February 23, 2017
"Utakapoenda kwa mtoa huduma ambaye unataka kuhamia utajaza fomu, atachukua taarifa zako na atatuma lile ombi unakohama"-@TCRA_Tz @cLOUDS
— millardayo (@millardayo) February 23, 2017
"Akishatuma taarifa kwa mtoa huduma ambako unahama, kwa kutumia simu yako utatuma ujumbe wenye neno HAMA kwenda 15080"@TCRA_Tz @Clouds360Tz
— millardayo (@millardayo) February 23, 2017
"Ombi lako la kuhama litakapokubalika, mtoa huduma atakupatia line ya simu mpya yenye namba ileile"- @TCRA_Tz @Clouds360Tz
— millardayo (@millardayo) February 23, 2017
"Zoezi la kuhama mtandao wa simu kwa namba ileile ni la hiari"-@TCRA_Tz @Clouds360Tz
— millardayo (@millardayo) February 23, 2017
"Kama kila kitu kipo sawa kwamba anayetaka kuhama mtandao hana tatizo lolote, zoezi litatumia chini ya dakika 15"-@TCRA_Tz @Clouds360Tz
— millardayo (@millardayo) February 23, 2017
"Ukihama kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine, kule ulikohamia unatakiwa ukae siku 30, baada ya siku 30 ndio unaruhusiwa kuhama"-@TCRA_Tz@
— millardayo (@millardayo) February 23, 2017
"Endapo utapiga simu kwenye namba ya mtu ambaye ameshahamia mtandao mwingine, utapata ishara ya milio miwili"- @TCRA_Tz @Clouds360Tz
— millardayo (@millardayo) February 23, 2017
"Huduma ya kuhama mtandao wa simu kwa namba ileile ipo nchi nyingi lakini ni kwa ajili ya nchi husika haivuki mipaka" –@TCRA_Tz @Clouds360Tz
— millardayo (@millardayo) February 23, 2017
"Kule unakohama haruhusiwi kuitoa namba ambayo umehama nayo, zikipita siku 90 haitumiki, ulikohamia watairudisha" @TCRA_Tz @Clouds360Tz
— millardayo (@millardayo) February 23, 2017
"Katika zoezi la kuhama, zile huduma zote zinazohusiana na kifedha zitasimamishwa, kabla hujahama hakikisha fedha zako umezitoa" @TCRA_Tz
— millardayo (@millardayo) February 23, 2017
"Zoezi la kuhama mtandao ni bure ila mtoa huduma atalazimika kukupatia laini mpya, kukutoza fedha ya laini itategemea na mtoa huduma@TCRA_Tz

AyoTVMAGAZETI: Bosi Polisi alivyouawa akiwavaa majambazi, wanafunzi 7,000 vyuo vikuu matatani, Ungana na Alice Tupa kwa kubonyeza play hapa chini