Stori za kukamatwa kwa meno ya tembo zimekua zikitoka kwa mfululizo nchini Tanzania ambapo kwenye post hii tunajiunga na Jeshi la Polisi 88.4 Mtwara ambalo lina taarifa za kukamatwa kwa watu wenye nyara za serikali alfajiri ya February 14 saa 11 katika kijiji cha Chungu kata ya Nanyumbu, tarafa ya Nanyumbu Mkoa wa Mtwara.
Taarifa inasema kuwa watu hao walikamatwa na polisi wakiwa kwenye kizuizi cha barabara ya Mtambaswala-Mangaka ambapo waliokamatwa ni pamoja na Hamidu Abdallah Ngunde (40), Dereva wa gari Geraldat Lukas (36) na Boniphace Kosan (29) wote wakazi 88.5 Dar es salaam.
Watuhumiwa hao walikua na jumla ya meno 58 yenye uzito wa jumla ya kilo 130.6 ambayo yana thamani ya shilingi Milioni mia saba za Kitanzania wakiwa wameyapakiza kwenye gari aina ya Toyota Land cruiser T208 AGC.
Unaambiwa mbinu waliyoitumia jamaa ni kukata floor ya chini ya Gari na kutengeneza tank la bandia na kuweka meno hayo kisha kuweka kapeti juu yake chini ya kiti cha kukalia abiria wa nyuma ya dereva, Jeshi la polisi Mtwara linawashikilia watuhumiwa wote watatu.
Taarifa kutoka Jeshi la Polisi Mtwara.