Wakati sakata la Vyeti fake likionekana kupungua baada ya Serikali kuchukua hatua katika Taasisi zake na Taasisi za Umma gumzo jingine limeibuka Mwanza leo June 16, 2017 baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ‘TAKUKURU’ kumkamata mtu aliyejifanya Mhandisi wa Jiji kisha kuomba rushwa.
Mkuu wa TAKUKURU Mwanza Erenst Makale amesema mtu mmoja anayefahamika kwa jina la James Edward ambaye ni Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mtakuja amekamatwa na Taasisi hiyo kwa kujifanya Mhandisi wa Jiji kisha kuomba rushwa ya Tsh. 200,000 kwa Mfanyabiashara.
>>>”Mtumishi huyu aliomba kwa Mfanyabiashara wa Zana za Kilimo ambaye Zana zake aliweka kwenye eneo ambalo ni Hifadhi ya Barabara…huyu mtu aka-take advantage (faida) akaenda kwake akijitambulisha kama Mhandisi wa Jiji. Akamtaka aondoe Zana zake za Kilimo au ampe Shilingi Milioni Moja. Katika kujadiliana, wakajadiliana wakashusha mpaka kwenye Laki Mbili.
“Mwananchi huyu akawa Muungwana akaja Ofisini kwetu. Tukafanya mtego tarehe 13, mtego huo ukafanikiwa lakini hela ilienda kupokelewa na Bwana Godfrey Joseph Mwangonda ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kata ya Mkolani. Mtu ambaye aliomba fedha ni Bwana James Edward Mwasemela ambaye ndiye Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mtakuja.
“Baada ya kumkamata tulikuja kubaini vitu vingine vya zaida kwamba mtu huyu James Edward Mwasemela ni sugu pamoja kwamba ni Mtumishi wa Umma lakini ameshiriki tena kwenye makosa mengine ya utapeli na kufunguliwa kesi mbili katika mwaka 2013 na 2016 na baadaye kesi hizo ziliondolewa…” – Erenst Makale.
Bonyeza PLAY kutazama VIDEO hii ina kila kitu…
Utafiti wa Twaweza kuhusu Utendaji na siasa Tanzania!!!