Mwimbaji Ommy Dimpoz amefunguka kuhusu kipindi alivyokuwa mgonjwa na kusema kuwa hakuwaza maisha ya muziki au kushindwa kuimba siku moja kutokana na tatizo la sauti, kikubwa kilichokuwa kikimfanya awaze ni vipi ataishi maisha yake ya kawaida.
Ommy Dimpoz amefunguka hayo kupitia mahojiano aliyoyafanya leo March 29,2019 na kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV.
“Sikuwaza kuimba niliwaza maisha yangu ya kawaida nitaishi vipi, Nilivyokuwa naumwa na sauti haitoki iliniumiza katika maisha ya kawaida nitaishi vipi maana kama nipo chumbani na mtu yupo sebuleni nitamuitaje anisikie na ukizingatia sauti ilikuwa ndogo na niliwaza ikija kupotea itakuaje, Sikuwaza kuimba kwa wakati ule ila niliwaza nitaishi vipi kwenye maisha haya ya kawaida” >>>Ommy Dimpoz
VIDEO: PIERRE KAONGEA LIVE VIDEO CALL NA VICTOR WANYAMA WA TOTTENHAM NA KAMPA SHAVU