Wakati Serikali ya Awamu ya Tano ikihimiza ujenzi wa uchumi kupitia viwanda, Kamishna Jenereli wa Magereza Tanzania Faustine Martine amezindua kiwanda cha kuchakata ngozi cha Jeshi la Magereza Mkoani Tabora.
Katika ufunguzi huo Mtaalam mwezeshaji wa kuchakata ngozi kutoka kiwanda hicho Abuu Shaban amemshauri Kamishna Mkuu wa Jeshi hilo kushirikiana na VETA kuwapatia vyeti wafungwa wanaomaliza muda wao.
“Hilo wazo ni zuri na tutafanya hivyo kwa lengo la kuwasaidia hawa Wafungwa wanaokuwa wamemaliza kutumikia vifungo vyao lakini wamepitia program ya urekebishaji na imewapatia ujuzi na kuwawezesha kupata kipato kwa njia ambazo ni halali” CGP Martine