Kwenye headlines za burudani wiki hii hatuwezi kuacha kuzitaja haedlines za T-Pain ambaye siku chache aliwatangazia mashabiki wake kuwa Album yake mpya Stoicville: The Phoenix itachelewa kutoka na badala ya kutoka mwisho wa mwaka huu, Album hiyo itakuwa sokoni mapema mwaka 2016.
Licha ya Album hiyo kuchelewa kutoka, T-Pain ameona aisogeze moja ya single zitakazopatikana kwenye Album hiyo… wimbo unaitwa ‘Or Wut’ na ndani msanii wa HipHop ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu kwenye headlines za burudani, Plies ameshirikishwa.
Kwenye interview yake na The Fader, T-Pain alisema, >>>”Wimbo huu sio kitu official sana bali ni kitu kidogo tu kwa ajili ya mashabiki wangu mpaka pale ntakapoiachia Album yangu mpya Stoicville: The Phoenix.”<<< T-Pain.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE kwa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE