Rais wa Klabu ya TP Englebert Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Moise Katumbi Chapwe ametajwa kuwa na mpango wa kuingia kwneye mbio za kuwania urais wa nchi hiyo unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Katumbi ambaye amekuwa Gavana wa jimbo la Katanga kwa muda mrefu amekuwa pia Rais wa Klabu ya TP Mazembe katika kipindi ambacho klabu hii imekuwa na mafanikio ikiwemo kutwaa ubingwa Ligi ya Mabingwa barani Afrika mara mbili mfululizo pamoja na kufika hatua ya fainali kwenye michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia.
Katumbi mwenyewe hajaweka wazi azma hii lakini vyanzo mbalimbali vya habari ambavyo viko karibu na Gavana huyu vimekuwa vimevujisha story kwamba mwaka mmoja kabla ya Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo, Katumbi atatangaza azma yake wazi kwa kila mtu.
Gavana huyu ametajwa kuungwa mkono na mamlaka kubwa Jijini Washington huku pia akiungwa mkono na wapinzani wakubwa wa Rais Joseph Kabila huku yeye mwenyewe akionesha kuwa na uhusiano mzuri na watu wa kambi ya upinzani.
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imekuwa chini ya Joseph Kabila tangu mwaka 2001 wakati baba yake mzazi Laureant Desire Kabila alipouawa na ameshinda uchaguzi katika miaka ya 2006 na 2011 huku kukiwa na shutuma za kuvurugwa kwa uchaguzi na ukosefu wa hali ya uchaguzi huo kuwa huru na wa haki.
Kikatiba Kabila hapaswi kugombea mwakani kwani anapaswa kukaa kwa mihula miwili pekee lakini rais huyo hadi sasa amekaa kimya na hajazungumza chochote hali ambayo imezua mijadala ya dhamira ya rais huyo kutaka kuongoza kwa awamu ya tatu.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos