Michezo

Samatta kaweka historia Ubelgiji, mchezaji wa tatu kuwahi kushinda Ebony Award 2019

on

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka katika club ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta nyota yake imezidi kung’aa baada ya kupata mafanikio siku hadi siku akiwa na club yake ya Ligi Kuu Ubelgiji.

Samatta usiku wa May 6 kuingia May 7 2019 amefanikiwa kutangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika 2019 anayecheza soka nchini Ubelgiji, tuzo ambayo inajulikana kwa jina maarufu la Ebony Shoe Award, Samatta anakuwa mchezaji wa tatu wa KRC Genk kuwahi kutwaa tuzo hiyo.

Mchezaji wa kwanza wa KRC Genk kuwahi kutwaa tuzo hiyo ni Souleymane Oulare raia wa Guinea ambaye alishinda tuzo hiyo 1999 na Moumouni Dagano raia wa Burkinafaso aliyeshinda tuzo hiyo 2002, pamoja na hayo Samatta hadi sasa anaongoza kwa ufungaji wa magoli ya Ligi Kuu Ubelgiji akiwa amefunga magoli 23 hadi sasa.

Pamoja na tuzo hiyo Samatta kwa sasa ni miongoni mwa wachezaji wenye mchango mkubwa katika club ya KRC Genk katika mbio za kuwania taji la Ligi Kuu Ubelgiji msimu wa 2018/2019 wakihitaji point 4 tu kuwa mabingwa pasipo kujali matokeo ya timu yoyote wakiwa wamesalia michezo mitatu na wana point 41.

Hata hivyo tuzo hiyo inayotolewa kwa mchezaji wa kiafrika au yoyote yule mwenye asili ya Afrika imewahi kuchukuliwa na wachezaji mbalimbali akiwemo mbelgiji Vincent Kompany anayeichezea Club ya Man City kwa sasa , Samatta hakuhudhuria utoajiwa tuzo hiyo kwa zile alizotaja kuwa ni sababu zilizo nje ya uwezo wake.

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments