Mamlaka ya mapato nchini(TRA) Mkoa wa Manyara imefikia asilimia 125 ya ukusanyaji wa mapato kwa robo ya kwanza ya mwaka huku ikiwataka wafanyabishara wenye mauzo ya shilingi milioni 11 kwa mwaka kutumia mashine za kieletroniki kutoa risiti.
Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya mlipa kodi Meneja wa TRA Mkoa wa Manyara Pendolake Msangi amesema mafanikio hayo ni kutokana na elimu inayoendelea kutolewa na mamlaka huku akiwatama watoa huduma kutoa risiti wanapouza bidhaa ili kuepuka adhabu pindi watakapo bainika kutoa tumia risiti hizo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange ambae ni Mwenyekiti ya ushauri ya Kodi wilaya ya Babati amesema shughuli ya kulipa kodi na utozaji wa Kodi inahitaji kushirikiana ambapo Serikali itaendelea kutoa elimu ya mlipa kodi ili kuendelea kulipa Kodi kwa hiari,huku watakaobainika kutotoa risiti za EFD kuchukuliwa hatua.