Top Stories

PICHA 5: Gari limechomwa mengine yamevunjwa Trump akiapishwa, ni hasira za wanaompinga

on

Mpaka usiku wa January 20 2017 Mamlaka kwenye taifa la Marekani zilisema wamekamatwa zaidi ya Waandamanaji mia moja (100) waliondamana kumpinga Rais mpya wa taifa hilo Donald Trump.

Maandamano yalisikika sana kwenye mji wa Washington DC alikoapishwa Donald Trump lakini baada yakasikika sehemu nyingine kama Austin Texas ambako wameandamana pia vilevile lakini hizi hapa chini ni picha kutoka Washington DC na zimeripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari.

Mpaka gari la Polisi limevunjwa kioo cha nyuma

Gari hili la kifahari lilichomwa moto ambapo Polisi na fire walipofika kwenye eneo la tukio walikuta tayari limewaka.

Waandamanaji wengine walionekana wakivunja vioo vya magari na maduka kwenye mitaa ya Washington DC.

ULIPITWA? Mume kaenda kazini Wife kaleta mchepuko nyumbani, tazama hapa chini kwa kubonyeza play

Soma na hizi

Tupia Comments