Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu wametolewa katika chumba cha Mahakama na kupelekwa katika mahabusu iliyopo mahakamani hapo baada ya kuwepo kwa hali ya sintofahamu kutokana na utaratibu uliotangazwa Mahakamani hapo na kupelekea kesi kuchelewa kuanza kusikilizwa.
Utaratibu mpya uliotangazwa Mahakamani leo ni kupunguza idadi maalum ya wanaofatilia kesi hiyo ambapo Mawakili walioruhusiwa ni 20, Waandishi wa Habari 10, Watu Maalum 3, Viongozi 5 na Ndugu 5.
Mabadiliko hayo yamefanya Jopo la Mawakili wa Freeman Mbowe kutoka nje ya chumba cha Mahakama, kupinga Wafuasi wa CHADEMA na Watu wengine kuzuiwa kuingia mahakamani, na Viongozi wa CHADEMA walioruhusiwa kugomewa kuingia na simu.
Sasa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara Tundu Lissu ameonesha kutokukubaliana na utaratibu uliopo Mahakamani leo wa Watu mbalimbali kuzuiwa kuingia na simu za mkononi kufuatilia kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na wenzake watatu.
TAZAMA WAFUASI WA CHADEMA WALIVYOZUILIWA KUINGIA MAHAKAMANI KUSIKILIZA KESI YA MBOWE NA WENZAKE