Good news ninayotaka kukusogezea kwa wewe mpenda burudani hususani muziki wa Afrika Kusini maarufu kama Amapiano ni kwamba warembo wanaounda kundi la liitwalo TXC akiwemo Tarryn & Clair wanatarajiwa kutua kwa mara nyingine katika ardhi ya Samia wikiendi hii.

Tarryn na Clair utakuwa ni ujio wao wa mara ya pili kuja Tanzania ambapo mnamo 11th July,2021 Jumapili hii wanatarajia kutoa burudani ya kuzicheza nyimbo zinazotamba kwasasa almaarufu kama Amapiano.

Wakali hao watazicheza live mbele ya watanzania watakaofika kwenye fukwe za Bahari maarufu kama Kidimbwi Beach iliyopo Mbezi ya chini karibu na Shoppers Plaza Dar es Salaam.

ULIIKOSA HII SUPRISE YA DARASSA YATAKA KUMTOA MACHOZI SHO MADJOZI JUKWAANI HUKU AKIWAIMBIA WATANZANIA KIDIMBWI BEACH