Habari za Mastaa

Utapenda kuiona hii mpya ya Ty Dolla Sign feat. Babyface; “Solid” – (Video)!

on

Wakati tukiwa tunaendelea kusubiri uzinduzi wa Album mpya ya Ty Dolla Sign ‘Free TC’ inayotegemea kuwa sokoni tarehe 13 November 2015, rapper huyo ameona aisogeze kwetu nyingine mpya kutoka kwake… baada ya kuachia ‘Saved’ wimbo uliosimamiwa na Producer DJ Mustard, Ty Dolla Sign safari hii anaileta kwetu ‘Solid’.

bbyface2

Ty Dolla Sign.

Kizuri kuhusu wimbo huu ni kwamba staa mkongwe wa muziki wa R&B Marekani, Babyface ameshirikishwa kwenye audio na video ya wimbo huu… kingine kuhusu album mpya ya Ty Dolla Sign, ndani ya Album hiyo mastaa wakubwa kama Kanye West, Kendrick Lamar, Wiz Khalifa, Future, R. Kelly na Trey Songz wameshirikishwa!

bbyface3

Babyface.

Japo imepita muda mrefu sana toka tumuone Babyface kwenye headlines za burudani, good news ni kwamba staa huyo yupo studio anamalizia Album yake mpya iliyopewa jina ‘Return Of The Tender Love’ itakayo kuwa sokoni tarehe 04 December 2015.

Hapa chini nimeisogeza kwako video ya Ty Dolla Sign, bonyeza play kuitazama.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments